06
Sep
Jinsi ya Kutambua Mafunzo Mapotovu
Katika Kipindi hiki, Esther Mwikali kutoka Biblia Husema Radio anamhoji Wanjiru Ng’ang’a ambaye ni mratibu wa Project Priscilla chini ya ACFAR Kenya. Esther anammuuliza Wanjiru baadhi ya maswali yakiwemo jinsi ambavyo wakristo wanaweza kutambua mafunzo potovu na vile ambavyo wanafaa kufanya baada ya kutambua ya kwamba wamekua wakifuata manabii au makanisa ya uongo.
Sikiliza kipindi hiki ili uweze kuelewa jinsi ambavyo utambuzi wa kibiblia ni dawa dhidi ya udanganyifu.